HOSPITAL YASHTUMIWA KUSABABISHA KIFO CHA MSANII WA BONGO MOVIEZ JOHN S. MAGANGA
Msanii wa bongo moviez john s masanga amefariki dunia jana saa 4 usiku
katika hospital ya mwananyamala kwa kile kilichosemakana kwamba alikuwa
ameanguka ghafla katika semina aliyokuwepo kwa ajili ya mambo ya
filamu.
Akiwa na kina natasha,mama yake monalisa na shija katika hali
isiyokuwa ya kawaida ameanguka gafla,na kukimbizwa katika hospital ya
mwananyamala hapo ndipo alipopimwa na kuambiwa kuwa alikua na vidonda
vya tumbo na kufanyiwa oparation, baada ya madaktar hao kuona kuwa hali
yake imezidi kuwa mbaya wakamwamishia hospital ya muhimbili na huko
ndipo alipoendelea kupata matibabu zaid, lakin hali yake ilizid kuwa
mbaya na kugundulika kuwa alikuwa na ugonjwa mwengine tofauti na
aliokutwa nao hospital ya mwananyamala.
Muhimbili waligundua kuwa alikuwa
na ugonjwa wa kujaa maji katika mapafu. ambapo muda wa kutibia ugonjwa
huo ulikuwa umeshakwisha mpaka kupelekea kifo chake. marehemu john s
maganga ameacha pengo kubwakatika tasnia ya filamu tanzania,marehemu
alishaigiza filamu nyingi kama;-mrembo kikojozi,chanzo ni mama, my
dreams,cake ya birthday,bar maid,pretty gal. na nyingine:
No comments:
Post a Comment