Bondia
wa kimataifa wa Marekani aliyepo jela kwa sasa Floyd Mayweather Jr.
ametajwa na jarida la Forbes kuwa ndio mwanamichezo anayeingiza fedha
nyingi kwa mwaka, akiwa amepeleka banki dola millioni 85,000,000 katika
kipindi cha miezi 12 iliyopita. Mayweather anafuatiwa na mpinzani wake
mfilipino Manny Pacquiao aliyeingiza kiasi cha $62 million.
Pamoja na
mchezo wa soka kuwa ndio maarufu zaidi lakini wacheza soka wenyewe
wameshindwa kuingia hata kwenye Top 5, ingawa wapo kwenye 10 bora.
Muingereza David Beckham akishika nafasi ya nane kwa kuingiza millioni
46 USD, huku akifuatiwa na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ambaye
amepeleka bank kiasi cha $42 million. Mchezaji bora wa dunia wa soka
Lionel Messi hayumo kwenye top 10, japo hayupo mbali akiwa nafasi ya 11
kwa kuingiza kiasi cha $39 million.



No comments:
Post a Comment